Sunday, January 15, 2012

Bomu lauwa watu 50 Iraq

14 Januari, 2012

Wakuu wa Iraq wanasema mtu aliyejitolea mhanga ameripua bomu na kuuwa watu kama 50, katika shambulio dhidi ya mahujaji wa Kishia katika mji wa Basra, kusini mwa nchi.

Inaarifiwa kuwa watu 90 wengine wamejeruhiwa.
Polisi walieleza kuwa mahujaji hao walikuwa wanaelekea msikiti mkubwa wa Washia nje ya Basra, mwisho wa ile wanayoita Arbain, moja kati ya vipindi vinavyoadhimishwa na Washia.
Askari wa usalama 7 ni kati ya watu waliokufa.
Shambulio hilo linakuja wakati mvutano wa kisiasa unazidi baina ya Washia, walio wengi Iraq, na Wasunii.
Mwezi uliopita, serikali yenye Washia wengi, ilitoa amri ya kumkamata makamo wa rais aliye wa madhehebu ya Sunni, Tariq al-Hashemi, kwa mashtaka ya ugaidi.

CHANZO: BBC Swahil

No comments:

Post a Comment